sw.wikipedia.org

Kihispania - Wikipedia, kamusi elezo huru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kihispania
Español
Castellano
Lugha
Asili Uhispania Puerto Rico Argentina, Bolivia, Chile, Colombia, Costa Rica, Cuba, Jamuhuri ya Dominican , Ecuador, El Salvador, Guinea ya Ikweta, Guatemala, Honduras, Meksiko, Nicaragua, Panama, Paraguay, Peru, Uruguay, na Venezuela.
Wasemaji

L1 : 500 Milioni
L2: 601 Milioni

Familia za lugha Kihindi-Kiulaya
Kilatini
Aina za Awali Kilatini ya kawaida
Kihispania cha Kale
Mfumo wa kuandika Kilatini
Nambari za Msimbo
ISO 639-1 es
ISO 639-2 spa
Glottolog stan1288

      Lugha ya Kwanza kwa wengi      Lugha Rasmi au Lugha ya Pili       Asilimia 20% kwenda juu

Kihispania (español) au Kicastilia (castellano) ni lugha ya Kiromansi kutoka familia ya lugha za Kihindi-Kiulaya, ambayo ilitokana na Kilatini cha Kawaida kilichozungumzwa katika Rasi ya Iberia huko Ulaya. Leo hii, ni lugha ya kimataifa yenye takriban wasemaji wa asili milioni 484, hasa katika Amerika na Hispania, na takriban milioni 558 wakiwemo wasemaji wa lugha ya pili. Kihispania ni lugha rasmi ya nchi 20, na pia ni moja ya lugha rasmi sita za Umoja wa Mataifa. Kihispania ni lugha ya pili duniani kwa idadi ya wasemaji wa asili baada ya Kichina cha Mandarin; lugha ya nne kwa idadi ya wasemaji duniani baada ya Kiingereza, Kichina cha Mandarin, na Hindustani (Kihindi-Kiurdu); na ndiyo lugha maarufu zaidi ya Kiromansi duniani. Nchi yenye idadi kubwa ya wasemaji wa asili ni Mexico.

Asili ya lugha hiyo ni katika nchi ya Uhispania (Ulaya kusini magharibi), lakini kutokana na historia ya ukoloni na ya biashara lugha hiyo imesambaa sana, hasa Amerika ya Kusini na ya Kati.

Lugha iliyozaa Kihispania ni Kilatini cha Waroma wa Kale waliotawala kwa muda mrefu Uhispania. Ndiyo sababu maneno yake yanatokana na Kilatini kwa asilimia 80, lakini pia na Kiarabu kwa asilimia 8.

Kati ya lugha za Kirumi Kihispania ni lugha ya kisasa ambayo ni karibu zaidi na lugha ya kale, isipokuwa Kisardinia na Kiitalia.

  • Nchini Marekani Kihispania ni lugha ya pili baada ya Kiingereza hasa katika majimbo ya Kusini zilizokuwa zamani sehemu za Mexiko.
  • Ufilipino kwa sababu ilikuwa koloni la Uhispania