sw.wikipedia.org

Kuchamsitu - Wikipedia, kamusi elezo huru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kuchamsitu
Kuchamsitu koo-njano
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia: Phylloscopidae (Ndege walio na mnasaba na kuchamsitu)
Alström, Ericson, Olsson & Sundberg, 2006
Ngazi za chini

Jenasi 2; spishi 16 katika Afrika:

Kuchamsitu ni ndege wadogo wa familia Phylloscopidae. Wanafanana na shoro, kucha na kuchanyika, na zamani wote waliainishwa pamoja katika familia Sylviidae. Spishi za Phylloscopus zina rangi ya kahawia au kijani mgongoni na nyeupe au njano chini. Zile za Seicercus zina rangi kali zaidi, kijani mgongoni na njano chini; zina milia kichwani na mviringo wa jicho mweupe au njano. Ndege hawa wanatokea misitu ya Afrika, Asia na Ulaya. Spishi zinazozaa katika kanda za halijoto ya wastani huhamia kusi, zile za Ulaya huenda Afrika. Hula wadudu. Hulijenga tago lao kwa umbo la kikombe ndani ya uoto mzito, mara nyingi karibu na ardhi. Jike huyataga mayai 2-7.

  • Kuchamsitu wa Bonelli

    Kuchamsitu wa Bonelli

  • Kuchamsitu wa Kanari

    Kuchamsitu wa Kanari

  • Kuchamsitu sauti-mbili

    Kuchamsitu sauti-mbili

  • Kuchamsitu mgongo-kahawia

    Kuchamsitu mgongo-kahawia

  • Kuchamsitu wa Hispania

    Kuchamsitu wa Hispania

  • Kuchamsitu nyusi-njano

    Kuchamsitu nyusi-njano

  • Kuchamsitu uso-mwekundu

    Kuchamsitu uso-mwekundu

  • Kuchamsitu mashariki

    Kuchamsitu mashariki

  • Kuchamsitu kiuno-njano

    Kuchamsitu kiuno-njano

  • Kuchamsitu mpigamluzi

    Kuchamsitu mpigamluzi

  • Kuchamsitu wa Ulaya

    Kuchamsitu wa Ulaya

  • Kuchamsitu kahawia

    Kuchamsitu kahawia

  • Arctic warbler

    Arctic warbler

  • Sulphur-bellied warbler

    Sulphur-bellied warbler

  • Radde's warbler

    Radde's warbler

  • Pale-legged leaf-warbler

    Pale-legged leaf-warbler

  • Greenish warbler

    Greenish warbler

  • Whistler's warbler

    Whistler's warbler