sw.wikipedia.org

Lambati wa Maastricht - Wikipedia, kamusi elezo huru

  • ️Sun Jun 12 2016

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mt. Lambati alivyouawa.

Lambati wa Maastricht (pia: Lambert, Lambertus, Lambrecht, Lambaer, Baer; Maastricht, leo nchini Uholanzi, 636 hivi – Liege, leo nchini Ubelgiji, 705 hivi [1]) alikuwa askofu wa Tongeren-Maastricht, kati ya Ubelgiji na Uholanzi kuanzia mwaka 670 hadi kifodini chake.

Alipopelekwa uhamishoni aliishi miaka saba katika monasteri ya Stavelot. Aliporuhusiwa kurudi jimboni[2], alifanya uchungaji kwa sifa njema.

Akishirikiana na Wilibrodi aliinjilisha kwa bidii eneo hilo, alimsaidia Landrada kuanzisha monasteri ya kike na alimlea Hubati wa Liege, mwandamizi wake [3].

Hatimaye aliuawa na wapinzani wake akiwa na Petro na Audolet, watoto wa ndugu yake waliojaribu kumlinda, labda kwa sababu alimlaumu mtawala kwa uzinifu wake [4].

Tangu kale wote watatu wanaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama watakatifu wafiadini[5].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 17 Septemba[6].

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.