sw.wikipedia.org

Nyuzilandi - Wikipedia, kamusi elezo huru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

(Elekezwa kutoka New Zealand)

Nyuzilandi
New Zealand (Kiingereza)
Aotearoa (Kimaori)
Bendera Nembo
Wimbo wa taifa
God Defend New Zealand (Mungu Ilinde New Zealand)

ukubwa_wa_picha

Eneo la Nyuzilandi

Mji Mkuu Wellington
Jiji kubwa Auckland
Lugha Rasmi
Kabila
  • 67.8% Waulaya
  • 17.8% Wamāori
  • 17.3% Waasia
  • 8.9% Wapasifiki
  • 3.0% Wengine
Aina ya Serikali Ufalme wa kikatiba
Gavana Mkuu Cindy Kiro
Waziri Mkuu Chris Hipkins
Ukubwa wa eneo
Jumla 268,680 km²
Idadi ya watu
Kadirio (2021) 5,132,870
Sensa (2018) 4,699,755
Msongamano 19.1 /km²
Pato la taifa PPP (2024)
Jumla increase $283.4 bilioni (ya 64)
Capita increase $52,980
Pato la taifa (2024)
Jumla increase $252.24 bilioni (ya 42)
Capita decrease $47,070
Kiashiria cha maendeleo ya watu (2019) 0.931 (ya 14)
Maendeleo ya Juu Sana
Kiashiria cha ukosefu wa usawa (2022)

30
Ukosefu wa usawa wa kati

Sarafu Dola ya Nyuzilandi
Eneo la saa (UTC +12) NZST
Nambari ya mwito +64
Jina la kikoa .nz

Nyuzilandi (kwa Kiingereza New Zealand kwa Kimaori: Aotearoa) ni nchi ya visiwani katika Pasifiki takriban km 1,500 upande wa mashariki-kusini wa Australia. Inajumuisha maeneo mawili makuu ya ardhi—Kisiwa cha Kaskazini (Te Ika-a-Māui) na Kisiwa cha Kusini (Te Waipounamu). Ni nchi ya visiwa ya sita kwa ukubwa kwa eneo na iko mashariki ya Australia kupitia Bahari ya Tasmania na kusini mwa visiwa vya New Caledonia, Fiji, na Tonga.

Eneo lake linaundwa na visiwa viwili vikubwa: Kisiwa cha Kaskazini (North Island au Te Ika-a-Māui) na Kisiwa cha Kusini (South Island au Te Waipounamu) na vingine 600 vidogo.

Miji mingine ni:

Idadi ya wakazi ni 4,690,000. Wengi wao (74%) bado wana asili ya Ulaya, ingawa asilimia yao inazidi kupungua. Wakazi asilia ni Wamaori waliotokea Polinesia na kuhamia visiwa hivyo kati ya miaka 1250-1300 BK; kwa sasa ni 14.9% ya wakazi wote. Wengine wana asili ya Asia (11.8%) na ya visiwa vya Pasifiki (7.4%).

Lugha rasmi ni Kiingereza, Kimaori na Lugha ya Ishara ya Nyuzilandi (kwa Kiingereza: New Zealand Sign Language au NZSL).

Upande wa dini, 49% ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali, kuanzia Kanisa Katoliki (12.6%), Anglikana (11.8%) na Wapresbiteri (8.5%). Idadi ya wasio na dini inazidi kupanda na imeshafikia 38.55%, mbali ya 12.27% wasiojibu swali kuhusu hilo. Kuna Mabanyani (2.1%), Wabuddha (1.5%), Waislamu (1.2%), Singasinga (0.5%)

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.