Oriensi - Wikipedia, kamusi elezo huru
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Oriensi (kwa Kifaransa: Orens; alifariki Auch, leo nchini Ufaransa, 450 hivi) alikuwa askofu wa mji huo na mshairi.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa kila tarehe 1 Mei[1].
Oriensi aliongoka baada ya kuishi katika dhambi akawa askofu mwenye sifa katika uchungaji wakati wa fujo zilizotokana na uhamaji wa makabila ya Kigermanik, akijitahidi kujenga amani kati yao na wenyeji, pamoja na kung'oa Upagani[2].
Alitunga utendi mrefu Commonitorium kuhusu maadili[3].
- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ Catholic Encyclopedia: Auch
- ↑ It exists in only one manuscript (Cod. Ashburnham. sæc. X), and is followed by some shorter anonymous poems not by Orientius, and by two prayers in verse attributed to him. The first complete edition was published by Martène, Veterum Scriptorum Monumenta, I (Rouen, 1700); then by Andrea Gallandi, Bibliotheca veterum Patrum, X (Venice, 1774), 185-96, reprinted by J.P. Migne in Patrologia Latina 61.977-1006. The best modern edition is by Ellis in the Corpus Scriptorum Eccl. Latinorum XVI (Vienna, 1888): "Poetæ Christiani minores", I, 191-261.
- Saint of the Day, May 1: Amator Ilihifadhiwa 21 Desemba 2010 kwenye Wayback Machine.
- Cathédrale Saint-Étienne (Image of St. Amadour)
- Procesión de San Amador, patrón de Martos (Jaén), el 5 de Mayo de 2006
![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |