Uturuki - Wikipedia, kamusi elezo huru
- ️Sun Feb 23 2025
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| ||||
Kaulimbiu ya taifa: Kituruki: Yurtta Sulh, Cihanda Sulh ("Amani nyumbani, amani duniani") | ||||
Wimbo wa taifa: İstiklal Marşı | ||||
![]() | ||||
Mji mkuu | Ankara 41°1′ N 28°57′ E | |||
Mji mkubwa nchini | Istanbul | |||
Lugha rasmi | Kituruki | |||
Serikali | Jamhuri Recep Tayyip Erdoğan | |||
Kuundwa kwa nchi ya kisasa Kuundwa kwa bunge Mwanzo wa vita ya uhuru Ushindi Kutangaza Jamhuri |
23 Aprili 1920 19 Mei 1919 30 Agosti 1922 29 Oktoba 1923 | |||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
783,562 km² (ya 37) 1.3 | |||
Idadi ya watu - [[]] kadirio - 2014 sensa - Msongamano wa watu |
{{{population_estimate}}} (ya 18 1) 77,695,904 101/km² (ya 107 1) | |||
Fedha | Lira Mpya2 (TRY )
| |||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
EET (UTC+2) CEST (UTC+3) | |||
Intaneti TLD | .tr | |||
Kodi ya simu | +90
- |
Uturuki, rasmi kama Jamhuri ya Uturuki (kwa Kituruki: Türkiye Cumhuriyeti), ni nchi inayopatikana kati ya Asia Magharibi na Ulaya ya Kusini-Mashariki, ikiwa na sehemu kubwa katika Anatolia na sehemu ndogo katika Thrace barani Ulaya. Inapakana na Bulgaria kaskazini-magharibi, Ugiriki magharibi, Georgia kaskazini-mashariki, Armenia, Azerbaijan (Nakhchivan), na Uajemi mashariki, Iraq na Syria kusini, na imezungukwa na Bahari Nyeusi kaskazini, Bahari ya Mediteranea kusini, na Bahari ya Aegean magharibi. Ina idadi ya watu takriban milioni 85, ikiwa ya 18 duniani. Jiji lake kubwa zaidi ni Istanbul, huku mji mkuu ukiwa Ankara. Uturuki imegawanyika katika mikoa 81. Inajulikana kwa historia yake tajiri kama sehemu ya Milki ya Ottoman, miji yake ya kale kama Efeso, Hagia Sophia, na umuhimu wake wa kijiografia kama kiunganishi kati ya Asia na Ulaya.
Jiografia

Sehemu kubwa ya mipaka yake ni bahari: Mediteranea upande wa magharibi na kusini na Bahari Nyeusi upande wa kaskazini. Kwenye nchi kavu imepakana na Ugiriki na Bulgaria upande wa magharibi, Kaskazini-mashariki na Georgia, Armenia na Azerbaijan, kwa upande wa mashariki na Iran na upande wa kusini na Iraq na Syria.
Sehemu kubwa ya eneo lake ni Anatolia inayoonekana kama rasi kubwa kati ya Mediteranea na Bahari Nyeusi. Hali ya nchi ndani ya Anatolia mara nyingi ni yabisi na kilimo kinategemea umwagiliaji.
Safu za milima zinafuatana na pwani za kusini na kaskazini.
Sehemu ya mashariki ya nchi kuelekea Uajemi na Kaukazi ina milima mingi.
Maeneo ya pwani yanapokea mvua na huwa na rutuba.
Historia
Waturuki waliwahi kuwa kiini cha Milki ya Osmani iliyounganisha mataifa mengi chini ya Sultani wa Konstantinopoli.
Uturuki wa kisasa umetokea kama nchi ya pekee baada ya vita viwili mwanzoni mwa karne ya 20.
Jamhuri ya Uturuki ilianzishwa mwaka 1923 na jenerali Kemal Atatürk baada ya vita vikuu vya kwanza, vilivyomalizika kwa kuvunja Milki ya Osmani, na vita vilivyofuata, vya kuondoa wanajeshi wa Ugiriki na nchi nyingine walioingia ndani ya sehemu iliyokuwa imebaki baada ya kuvunjika kwa dola kubwa.
Atatürk alileta mabadiliko mengi yaliyolenga kuondoa utamaduni wa kale wa Waosmani na enzi za utawala wa sultani wa Kiislamu.
Magharibi ya nchi imeendelea sana lakini maeneo ya mashariki yamebaki nyuma.
Nchi ya kisasa
Siku hizi Uturuki unalenga kuingia katika Umoja wa Ulaya.
Serikali ina utaratibu wa kidemokrasia ya vyama vingi. Utawala wa nchi ni kwa mikoa 81.
Mji mkuu ni Ankara ulioko katika kitovu cha Anatolia.
Mji mkubwa ni Istanbul ulioitwa zamani Konstantinopoli na zamani zaidi Bizanti: ulikuwa mji mkuu wa Dola la Uturuki hadi mwaka 1923.
Demografia
Uturuki una wakazi zaidi ya milioni 76. Wengi wao (70-75%) ni Waturuki. Katika mashariki ya Uturuki watu wengi ni Wakurdi ambao ni milioni 14 au takriban 20% za raia wote wa Uturuki.[1]
Kuna mabaki madogo tu ya Wagiriki na Waarmenia waliowahi kukalia sehemu kubwa za nchi hadi mwisho wa milki ya Osmani.
Kwenye maeneo jirani na Syria wako pia Waarabu.
Lugha rasmi na ya kawaida ni Kituruki, kinachotimika na 85% za wakazi. Hata hivyo, lugha 36 huzungumzwa nchini Uturuki, yaani 14 za asili na 22 za nje (angalia orodha ya lugha za Uturuki).
Upande wa dini, karibu wote ni Waislamu, hasa kuanzia karne ya 20 ambapo Wakristo wengi waliuawa (hasa Waarmenia) au kuhama (hasa Wagiriki). Waliobaki ni 0.2% tu. Hata hivyo Uturuki ni nchi isiyo na dini rasmi.
Picha za Uturuki
-
Ayasofya (zamani: Kanisa la Hagia Sofia) mjini Istanbul wakati wa usiku
-
Misikiti Selimiye (Edirne)
Tazama pia
Viungo vya nje
- Jumla
- turkey.com - Topical multilingual website about Turkey.
- Turkey entry at The World Factbook
- Turkey profile from the BBC News
- Turkey at Encyclopædia Britannica
- Turkey Ilihifadhiwa 9 Juni 2012 kwenye Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- Uturuki katika Open Directory Project
- Key Development Forecasts for Turkey from International Futures
- Serikali
- Official website of the Presidency of the Republic of Turkey Ilihifadhiwa 5 Juni 2010 kwenye Wayback Machine.
- Official website of the Grand National Assembly of Turkey Ilihifadhiwa 23 Januari 2015 kwenye Wayback Machine.
- Utalii
- Wikimedia Atlas of Turkey
- Turkey's Official Tourism Portal Ilihifadhiwa 5 Julai 2008 kwenye Wayback Machine.
- Official website of the Ministry of Culture and Tourism
- Turkey profile from UNESCO
- Turkey profile from Lonely Planet
- Uchumi
- Official website of Ministry of the Ministry of Economy Ilihifadhiwa 1 Novemba 2015 kwenye Wayback Machine.
- Macroeconomic Data for Turkey Online Ilihifadhiwa 17 Novemba 2014 kwenye Wayback Machine.
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Uturuki bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Uturuki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
- ↑ Worldometers. "Demografia za Uturuki" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-02-23.