Wasomali - Wikipedia, kamusi elezo huru
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maeneo penye idadi kubwa kiasi |
---|
Pembe ya Afrika |
Lugha |
Dini |
Karibu wote: Uislamu (Sunni, Sufi) |

Wasomali ni kabila kubwa la watu wa jamii ya Wakushi wanaoishi katika eneo linaoitwa Pembe ya Afrika ambalo ni eneo linalopakana na Bahari ya Hindi na kugawanyika kati ya nchi asili nne: Somalia, Kenya, Ethiopia na Jibuti.
Idadi ya Wasomali walioko Somalia ni kama milioni 15, Ethiopia milioni 8.5, Kenya ni karibu milioni 2.5 au 3 [1] na Jibuti zaidi ya nusu milioni. Walioko nje ya eneo asili pia ni wengi, hasa huko Yemen. Jumla yao ni milioni 28-30.
Lugha yao ni Kisomali, mojawapo kati ya lugha za Kikushi.
![]() |
Makala hii kuhusu utamaduni wa Kenya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wasomali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |