Wasunni - Wikipedia, kamusi elezo huru
Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya |
Imani na ibada zake |
Umoja wa Mungu |
Waislamu muhimu |
Abu Bakr • Ali |
Maandiko na Sheria |
Qur'an • Sunnah • Hadithi |
Historia ya Uislamu |
Tamaduni za Kiislamu |
Shule • Historia |
Tazama pia |
Wasunni ni dhehebu kubwa ndani ya dini ya Uislamu. Takriban asilimia 80 - 90 za Waislamu wote duniani hukadiriwa kuwa Wasunni na wengine 10-20 % huhesabiwa kati ya Washia.
Wasunni huitwa kwa Kiarabu ahl ul-sunna (Kiarabu: أهل السنة; "watu wa mapokeo"). Neno Sunni hutokana na neno sunna (kwa Kiarabu : سنة ) inayomaanisha mapokeo ya Mtume Muhammad.
Isipokuwa Uajemi, Iraki, Bahrain, Azerbaijan, Yemen, Omani na Lebanoni kundi hilo ni kubwa katika nchi zote penye Waislamu wengi.
Historia[hariri | hariri chanzo]
Wasunni hufuata mwelekeo wa Uislamu ulioanzishwa na ukhalifa wa Abu Bakr na kutokubali uongozi wa familia ya Mtume Muhammad kupitia Ali, Hassan na Husain.
Madhehebu ya Wasunni[hariri | hariri chanzo]
Kati ya Wasunni kuna madhehebu nne zinazotofautiana kiasi kuhusu mafundisho ya sharia au sheria ya kidini ya Kiislamu. Ndio Wahanafi, Wamaliki, Washafii na Wahanbali. Kwa jumla Wasunni hukubaliana ya kwamba madhehebu haya yote manne ni sawa.
Walimu wengine hasa katika kikundi cha Wawahabi kilichoanzishwa kati ya Wahanbali kimekaza mafundisho yake hadi kuwashtaki wengine kuwa si Waislamu wa kweli.